Ligi Ya WanawakeNyumbani

Yanga Princess yalamba udhamini Mil 120/-

Timu ya soka ya wanawake ya Yanga Princess leo imeingia mkataba na Kampuni ya Watercom kama mdhamini wa klabu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mtendaji Mkuu klabu ya Yanga, Andre Mtine.

Akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba huo Mtendaji mkuu klabu ya Yanga Andre Mtine amesema Hiyo ni hatua kubwa na inaonesha kwa jinsi gani klabu imejipanga kuboresha masuala ya kiuchumi.

“Leo ni siku muhimu sana kwetu kwenye maendeleo ya mpira. Ninajivunia kuona nasaini mkataba mpya kwa niaba ya Klabu,”amesema Mtine.

Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said amesema kwa miaka mingi vilabu hapa nchini vimekuwa vikikumbana na adha mbalimbali za kiuchumi na hii inatokana na kukosekana mikakati imara ya kuwashawishi wadhamini.

Eng. Hersi amesema: “Huu ni muendelezo wa ajenda yangu kubwa ya kuimarisha timu kiuchumi, na kwa kupitia mkataba huu tunaendelea kuimarisha hali yetu ya kiuchumi ili kuwa imara zaidi.”

Mkataba huo una thamani ya sh milioni 120 sawa na milioni 10 kwa mwezi ambapo kampuni hiyo pia itatoa katoni 1500 za maji kwa mwezi pamoja na vinywani vingine vyenye thamani ya jumla ya Sh milioni 50 kwa klabu hiyo kwa mwaka.

Rais wa Yanga, Eng. Hersi Said(kulia) Mkuu wa Kitengo cha masoko cha Watercom Mohamed Salim (kushoto).

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha masoko cha Watercom Mohamed Salim amesema ni heshima kubwa kwa kampuni hiyo kupata fursa hiyo ya kufanya kazi tena na Yanga.

“Mkataba wetu huu wa mwaka mmoja hatuna wasiwasi na tuna “Timu ya Yanga Princess ni timu kubwa ambayo ina malengo ya kuweka historia kubwa kama ambavyo ipo Yanga SC ambayo inahistoria ya kipekee,” amesema Salim.

Related Articles

Back to top button