U20

Shime awapongeza Twiga Stars

Kocha wa time ya taifa ya Wanawake ‘Twiga Stars’ Bakari Shime,  amewapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kujitoa na kurudi na ubingwa wa Kombe la Cosafa.

Akizungumza hivi karibuni kocha huyo amesema wachezaji wake walicheza kwa kujitolea kwa maslahi ya taifa lao la Tanzania hivyo hawanabudi kupongezwa kwa juhudi walizozionesha.

“Niwapongeze wachezaji wangu na timu nzima ya benchi la ufundi ukweli mashindano hayakuwa mepesi ispokuwa ni juhudi za wachezaji wangu kwa kufuata vizuri maelekezo tuliyokuwa tukiwapa ndani ya uwanja, ” amesema Shime.

Amesema timu yao bamoja na ubora iliyouonesha lakimi hawakuwa na maandalizi mazuri kama ilivyokuwa kwa baadhi ya timu kama wenyeji Afrika Kusini na Zambia.

“Uwezo walionao wachezaji wetu pamoja na njaa ya mafanikio ndio vimetusaidia lakini wenzetu Afrika Kusini na Zambia walikuwa vizuri kwenye maandalizi ukilinganisha na baadhi ya nchi nyingine tukiwemo na sisi, “.

Kocha huyo pamoja na yote pia amelipongeza Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF,   kwa juhudi zao za kufanikisha waweze kwenda kushiriki michuano hiyo huku wakikabiwa na mchezo wa kufuzu michuano ya kombe la dunia kwa timu ya Wanawake chini ya umri wa miaka 20 dhidi ya Eritrea ambao walilazimikakuigawa timu makundi mawili na kote wakafanikiwa kufanya vizuri.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button