Kivumbi fainali Europa Conference leo
FAINALI ya Ligi ya Europa Conference inafanyika leo kati ya Olympiacos na Fiorentina.
Kipute hicho kitapigwa kwenye uwanja wa OPAP uliopo mji mkuu wa Ugiriki, Athens kikiamuliwa na mwamuzi wa kati Artus Dias wa Ureno.
Katika kufunga msimu wa ulaya, tayari fainali ya Ligi ya Europa imefanyika Dublin, Ireland huku Atalanta ukinyakua ubingwa kwa kuichapa Bayer Leverkusen mabao 3-0.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itakamilisha msimu huo kwa mchezo kati ya Borussia Dortmund na Real Madrid Juni Mosi kwenye uwanja Wembley, Jijini London, England.