Nyumbani

Yanga sasa kusalia Avic

DAR ES SALAAM: YANGA wabadilisha gia baada ya kuweka wazi kuwa hawataenda nje ya nchi kuweka kambi, kama ilivyokuwa mipango yao ya awali na kuendelea kusalia Avic Town, jijini.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema mipango yao ya awali ilikuwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kuweka kwa ajili ya maandalizi (Pre Seasson), mambo yamebadilika na wataendelea kusalia Tanzania.

Mipango ya ilikuwa kwenda nchini Afrika Kusini kwa ajili ya maandalizi ya msimu wa 2024/25 pamoja na kucheza mechi kulingana na programu ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Miguel Gamondi.

“Tulikuwa na mipango ya kwenda nje ya nchi kwa ajili ya Pre Seasson, tutabaki Avic Town, tukijiandaa kwa msimu mpya wa mashindano, tunaweza kusafiri kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Kaizer Chiefs, katika kombe la Toyota,” amesema Kamwe.

Ameongeza kuwa misimu yote wanayofanya vizuri timu yao inatokea katika kambi hiyo na wanaimani wanapotekea Avic Town, wanafanikiwa katika mipango yao ikiwemo kufanya vizuri kwenye ligi ya ndani na michuano ya kimataifa kwa kucheza robo fainali.

Kuhusu usajili, Kamwe amesema unaendelea kuboresha kwenye nafasi zilionekana zina mapungufu kwa kufuata ripoti na mapendekezo ya Gamondi kuimarisha kikosi cha Yanga kwa ajili ya kuleta watu watakaofanikiwa kwenye mipango yao ya kucheza fainali ya ligi ya mabingwa Afrika.

Related Articles

Back to top button