Shamra Shamra za Yanga na Simba siku ya Dabi

DAR ES SALAAM: SHAMRA SHAMRA za mashabiki wa timu zote mbili Yanga na Simba, uwanja wa Benjamin Mkapa kila mmoja akiwa na muonekana wa jezi za timu yao pendwa.
Mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam na mikoani ikiwemo Arusha, kundi maarufu la wadudu walijitokeza kwa wingi katika uwanja wa Benjamini Mkapa unaobeba mashabiki 60,000 kushuhudia Dabi hiyo ya mchezo wa Ngao ya Jamii kutafuta mshindi mmoja atakayekwenda fainali.
Mshindi wa mchezo huo sasa atakutana na Azam FC ambaye ameibuka na ushindi mnono wa mabao 4-2 dhidi ya Coastal Union mchezo uliopigwa katika dimba la New Amaan complex Zanzibar
Usalama:
Mechi za dabi mara nyingi zinakuwa na mashabiki wengi, jeshi la polisi limeweza kuimarisha usalama wa watu na mali zao kwa kuwepo kwa farasi wanne walioingia uwanjani tofauti na ilivyo kwa matamasha ya Simba na Yanga ambao walikua nje.
Licha ya kuwepo kwa farasi hao lakini polisi walikuwa kila eneo kuhakikisha mashabiki wanakuwa na amani kushuhudia dabi hiyo.
Ndani ya uwanja hadi kufikia sasa inaonyesha mashabiki wa Yanga wameonekana kuwa wengi tofauti na wapinzani wao, huenda imechagizwa kwa kufanya vizuri katika mechi za hivi karibuni za dabi.