Ligi Kuu

Azam FC yakanusha kupokea maombi ya Ibenge

DAR ES SALAAM: OFISA Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema klabu hiyo haijapokea taarifa yoyote rasmi kuhusu kuhitajika kwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Florent Ibenge, kutoka klabu nyingine zinazotajwa kumwania.

Ibwe amesema pia kocha huyo mwenyewe hajawasilisha taarifa yoyote kwa uongozi wa Azam FC kupitia wawakilishi wake kuhusu nia ya kuondoka au kuhitajika mahali pengine.

“Kama klabu hatujapokea taarifa zozote kutoka kwa mwalimu au timu zinazotajwa kumuhitaji,” amesema Ibwe.

Kauli hiyo imekuja wakati kukiwa na taarifa zinazoendelea kusambaa zikihusisha kocha huyo na uwezekano wa kujiunga na baadhi ya timu za taifa barani Afrika kutokana na mafanikio yake akiwa na Azam FC na timu mbalimbali alizowahi kupitia.

Ibwe amesisitiza kuwa hadi sasa Ibenge anaendelea na majukumu yake ya kawaida ndani ya klabu hiyo.

Florent Ibenge ameendelea kuwa mmoja wa makocha wanaoheshimika barani Afrika kutokana na uzoefu wake mkubwa pamoja na mafanikio aliyowahi kuyapata katika timu mbalimbali alizozinoa.

Related Articles

Back to top button