Ligi Ya WanawakeNyumbani
Mtifuano dabi ya Kariakoo wanawake

MICHEZO mitano ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara(SLWPL) ukiwemo dabi ya kariakoo kati ya Yanga Princess na Simba Queens inapigwa leo kwenye viwanja tofauti.
Mchezo huo wa dabi ya kariakoo kwa wanawake utapigwa uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katika mchezo wa kwanza kati ya Yanga Princess na Simba Queens uliopigwa Desemba 22, 2022 timu hizo zilitoka sare ya goli 1-1 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.
Michezo mingine ya SLWPL ni kama ifuatavyo:
Baobab Queens vs JKT Queens
Amani Queens vs Ceasiaa Queens
Mkwawa Queens vs Fountain Gate Princess
Alliance Girls vs The Tigers Queens