Habari MpyaLigi Daraja La Kwanza

Simba inaandaa timu katili sana

DAR ES SALAAM: WAKATI Simba ikimtambulisha kiungo Mkabaji, Yusuph Kagoma, Mwekezaji na Mwenyekiti wa Simba, Mohammed Dewji (Mo), amesema wamefanya usajili kwa kushirikiana na benchi la ufundi na maskati kutoka mataifa zaidi ya 50, kujenga timu imara kwa msimu wa 2024/25.

Simba wamemtambulisha rasmi Kagoma baada ya kusaini mkataba wa miaka mitatu akitokea Singinda Fountain Gate, nyota huyo amekuwa akihusishwa kufanya mazungumzo na Yanga.

Mwenyekiti wa bodi ya Simba SC Mo Dewji amesema kuwa wamefanya usajili kulingana na mapendekezo ya benchi la ufundi kwa kushirikiana na kocha wao, Fadlu David na maskauti kutoka mataifa mbalimbali kulingana na aina ya wachezaji wanaowahitaji kufikia malengo ya timu kulingana na mipango mkakati .

“Jana kwa mara ya kwanza nimekutana na wachezji wote tuliowasajili na benchi nzima la ufundi la Simba, kuzungumza nao mambo mbalimbali ikiwemo mipango yetu kuelekea msimu ujao ninaimani tutafanya vizuri,” amesema Mo Dewji.

Ameongeza kuwa kikosi hicho kitaondoka nchini leo jioni kuelekea nchini Misri, kuweka kambi ya siku 24 hadi 25 na kurejea mwishoni mwa Julai, 2025 kwa ajili ya maandalizi ya simba Day inayotarajiwa kufanyika Agosti 3, mwaka huu.

“Tumesajili vizuri tumezingatia mahitaji ya timu na benchi la ufundi, tumeridhishwa na wachezaji tuliowasajili, ninaimani kubwa Pre Seasson wachezaji watapata muda wa kuzoeana na na Kocha Fadlu atapata nafasi ya kuandaa timu yake kwa utulivu,” amesema Mwenyekiti huyo.

Meneja wa Idara ya habari na mawasiliano, Ahmed Ally amesema kikosi kinaondoka leo jioni na kipa wao namba moja, Ayoub Lakred ataungana na timu moja kwa moja nchini Morocco.

“Safari ni leo, wachezaji ambao hawajapata nafasi ya kuondoka itakuwa wamechelewa kupata vibali hadi Jumatano hii wote watawakuwa wamewasili nchini Misri na kuanza rasmi maandalizi ya msimu mpya,” amesema Ahmed.

Related Articles

One Comment

  1. Pingback: Homepage
Check Also
Close
Back to top button