EPL

Spurs kumkingia kifua Bentancur

LONDON: Tottenham wanatarajia kukata rufaa kupinga adhabu ya kufungiwa mechi 7 ya kiungo wao wa kati Rodrigo Bentancur kutokana na matamshi ya yaliyoonekana ya kibaguzi aliyoyatoa kuhusu mchezaji mwenzake wa Spurs Heung-Min Son katika mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nyumbani kwao Uruguay mwezi Juni mwaka huu.

Mtangazaji wa kituo hicho alimuomba Kiungo huyo wa zamani wa Juventus aoneshe jezi ya mchezaji wa Spurs na akajibu: “Ya Sonny? Inaweza kuwa ya binamu yake pia kwa sababu wanafanana kama ndizi.”

Ingawa Bentancur aliomba radhi haraka uamuzi wa haraka wa jopo la tume huru ya udhibiti na usimamizi wa wachezaji ulihitajika aidha kuunga mkono au kupinga adhabu ya chama cha soka cha England FA.

Son alisema yeye na Bentancur walibaki kuwa “ndugu” baada ya matamshi hayo na “hakuna kilichobadilika” baada ya raia huyo wa Uruguay kukubali alichofanya ni kosa na kumuomba radhi.

Tottenham itasafiri hadi Manchester kukipiga na wenyeji wao Manchester City Jumamosi hii ya Novemba 23, kisha kukiwasha dhidi ya AS Roma kwenye Europa league na baadae kuvaana na Fulham, Bournemouth na Chelsea michezo ambayo Bentancur atakosekana kutokana na adhabu hiyo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button