Rodri autamani msimu wa 2024/25
MANCHESTER: KIUNGO wa Manchester City Rodrigo Hernández Cascante ‘Rodri’ amesema analenga kurejea uwanjani kabla ya msimu huu kutamatika baada ya kukaa nje kwa muda kutokana na jeraha baya la goti lililotabiriwa kumuweka nje msimu mzima alilopata mwezi Septemba.
Rodri, ambaye alishinda tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia ya Ballon d’Or mwezi uliopita, alifanyiwa upasuaji baada ya kupata jeraha la anterior cruciate ligament wakati wa sare ya 2-2 na Arsenal, huku meneja Pep Guardiola akisema hatacheza tena msimu huu.
“Lengo langu ni kurejea msimu huu, Nadhani kimawazo yangu itakuwa vizuri kwangu kutoukatia tamaa msimu huu na kuutupa. Sijui ni lini … lengo langu ni miezi sita au saba, lakini madaktari wangu wa viungo, wataamua” Rodri (28) aliambia podikasti ya “The Rest is Football” katika ‘episode’ kilichochapishwa leo.
Manchester City wamekuwa na wakati mzuri sana wakiwa na kiungo hyo na wameonekana kuchechemea kipindi hiki ambacho ni majeruhi. Mabingwa hao watetezi ni wa pili kwenye msimamo wa Ligi ya kuu ya England na watapania kupunguza pengo la pointi nane nyuma Liverpool watakapowatembelea vinara hao Jumapili hii.