Bayern yahamia kwa Olise
BAYERN MUNCHEN imewasiliana na Crystal Palace usiku wa kuamkia leo kuona uwezekano wa kunasa saini ya kiungo Mfaransa, Michael Olise.
Palace pia wamearifiwa kuhusu uamuzi wa Olise wa kujiunga na Mabavari hao huku baadhi ya vipengele binafsi vikiwa vimekubaliwa.
Imeripotiwa kutoka kwa Fabrizio Romano kuwa dau la mwisho la nyota huyo ni takriban £50m kama ada ya jumla ya Palace.
Hatua hiyo imetokana na Chelsea kujiondoa katika mbio za kumsajili mchezaji huyo baada ya taarifa kuwa Palace wameamua kumpa mkataba mpya na kiwango cha juu cha mshahara.
Kwa mujibu wa David Ornstein, Newcastle na Man United ni miongoni mwa klabu zinazowania saini ya mchezaji huyo.
Pia imeelezwa Bayern wametoa ofa nyingine kwa kiungo wa Fulham Joao Palhinha, kiasi cha £40m kinatajwa kutaka kufanya uhamisho wa mchezaji huyo.
Olise amefunga mabao 10 na kutoa pasi za mabao sita katika michezo 19 ya msimu wa 2023/2024 akiwa na Palace. Msimu umeisha akiwa hana kadi nyekundu wala njano.