Panga kali kupita Chelsea

TIMU ya Chelsea inapanga kuachana na idadi kubwa ya wachezaji wa kikosi cha kwanza baada ya kukamilisha kusajili 16 wapya tangu Todd Boehly na Learlake walipoichukua timu hiyo majira ya joto yaliyopita.
Chelsea ambayo imekubali dili kumsajili Christopher Nkunku kutoka RB Leipzig majira yajayo ya joto pia itapokea ofa kwa ajili ya kuwauza Christian Pulisic, Kalidou Koulibably, Mateo Kovacic na Pierre-Emerick Aubameyang.
Ripoti zimesema klabu ya Inter inasubiriwa iwapo itamchukua Romelu Lukaku kwa msimu mwingine kwa mkopo.
Huenda Callum Hudson-Odoi asiendelee kubaki Chelsea atakaporejea klabu hiyo akitokea Bayer Leverkusen alikokwenda kwa mkopo.
Inaeleweka kwamba Arsenal inamfuatilia Hudson-Odoi wakati Manchester City inahusishwa na Ben Chilwell.
aidha huenda Conor Gallagher akalazimika kutafakari hatma yake baada ya ujio wa Enzo Fernandez.
Kazi kubwa ya Chelsea sasa ni kukubaliana dili mpya na Mason Mount ambaye amebakiza miezi 18 katika mkataba wake.
Liverpool inaweza kutuma ombi kumsajili Mount majira yajayo ya joto iwapo mazungumzo ya Chelsea na kiungo huyo yatakwama.