Mastaa

Cassie aaga Marekani baada ya kulipwa zaidi ya bilioni 2.5 kutoka kwa Didy

NEW YORK: MPENZI wa zamani wa mwanamuziki Sean Combs (P.Didy), Cassie Ventura maarufu Cassie ameweka wazi kuwa kwa sasa hana mpango wa kurejea kuishi nchini Marekani baada ya kuhama nchi hiyo.

Mwanadada huyo ambaye pia ni mwimbaji na mwanamitindo maarufu amesema uamuzi huo ameupata baada ya miaka mingi ya misukosuko ya kisheria iliyomuhusisha aliyekuwa mpenzi wake, Sean ‘Diddy’ Combs.
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakama zilizowasilishwa hivi karibuni. Kauli hiyo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wake ambao wamekuwa wakifuatilia maisha yake tangu aibuke na madai ya unyanyasaji dhidi ya Diddy.

Hatua hiyo inakuja miaka michache baada ya Cassie kufikia makubaliano ya mabilioni ya fedha na Diddy kufuatia kesi ya madai aliyokuwa amefungua dhidi yake.

Ripoti zinaeleza kuwa alilipwa takribani dola milioni 20, sawa na zaidi ya Shilingi bilioni 2.5 za Tanzania.

Mbali na makubaliano hayo, Cassie pia aliripotiwa kupata fidia nyingine ya dola milioni 10 kutoka hoteli moja jijini Los Angeles kutokana na tukio lililonaswa na kamera za usalama.

Hata hivyo, jina lake limeendelea kujitokeza katika kesi nyingine mpya inayomhusisha Clayton Howard, mwanaume anayejitambulisha kama escort na ambaye anadai aliwahi kushiriki katika shughuli zilizowahusisha Cassie na Diddy.

Licha ya madai hayo mapya kuendelea mahakamani, Cassie ameonekana kuendelea na maisha yake mapya mbali na macho ya wengi kumtazama kwa namna tofauti za sintofahamu kutokana na uamuzi wake huo.

Mahali alipo kwa sasa hakujatajwa rasmi, lakini nyota huyo anaonekana kuamua kuanza ukurasa mpya wa maisha yake nje ya Marekani.

Related Articles

Back to top button