Riadha
Riadha Iringa yapata uongozi mpya

IRINGA:CHAMA cha Riadha mkoa wa Iringa kimepata viongozi wapya katika uchaguzi Mkuu uliofanyika jana.
Viongozi waliochaguliwa ni Mwalimu Yusuf Fute (Mufindi) Mwenyekiti, Jesca Mahoro(Mufindi), Makamu Mwenyekiti, Baha Qamunga (Iringa ) Katibu, Maltida Iswente (Mufindi) na Katibu msaidizi, Prosper Mwelele(Iringa).
Mhazini ni Abdallah Musa (Iringa ) mjumbe mkutano mkuu, na wajumbe watatu wa kamati tendaji ni Fabiani (Mafinga Mji), Joseph Hali (Kilolo), na Samweli Komba (Iringa ).
Matokeo hayo yametangazwa na Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ikiongozwa na Mwanasheria Oscar Daudi, Katibu Valentine Msuva na Dk Chachage.
“Iringa tumeungana kwa maslahi ya Riadha,” Tunaanza safari ya matumaini,”ilisema taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi.