Riadha

RT yaita vijana kwenye majaribio April 19

DAR ES SALAAM: SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT) limeita vijana wa michezo ya miruko na mitupo chini ya umri wa miaka 18 na 20 kujitokeza kwa majaribio kuchagua timu ya Taifa.

Akizungumza Dar es Salaam na SpotiLeo Katibu Mkuu wa RT Wakili Jackson Ndaweka amesema majaribio hayo yatafanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa April 19, mwaka huu.

Amesema lengo la majaribio haya ni kuchagua timu itakayowakilisha nchi katika mashindano ya vijana ya Afrika Mashariki ya umri huo yatakayofanyika April 25 na 26, Tanzania ikiwa mwenyeji kwenye Uwanja wa Mkapa.

“Tunatarajia mikoa yote ya Tanzania bara ilete wachezaji, Zanzibar wao kwenye mashindano ya Afrika Mashariki watashiriki kama nchi. Michezo itakayohusishwa ni ya viwanjani, miruko kukimbia, kukimbia na mitupo,”amesema.

Amesema kutakuwa na mita 100, 200, 400, 800, 1500 na 5000 kwa vijana wanawake na wanaume kwa umri chini ya miaka 18 na 20.

Ndaweka amesema wanataka kuwajaribu viwango vyao kujua kama wanaweza kuwakilisha nchi. Amesema mbio za viwanjani lazima wafanye majaribio na kwamba wale watakaochaguliwa watawekwa kambini kujiandaa na mashindano hayo ya Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button