Ulega ataka wasichana wapewe nafasi michezoni
DA ES SALAAM: WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega, amewataka watanzania kupinga mila potofu zinazokwamisha ushiriki wa wasichana katika michezo.
Amesema waunge mkono juhudi na wawape nafasi ya kushiriki michezo mbalimbali ikiwa ni faida kwa jamii na Taifa kwa kuwa michezo ni ajira.
Ulega ni mgeni rasmi katika ufunguzi wa mashindano ya sita ya Riadha ya wasichana chini ya miaka 20 (Ladies First) ambayo yanatafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia leo Novemba 23 na 24 mwaka huu.
Amesema endapo wasichana na vijana wa kiume watapewa nafasi ya kushiriki katika michezo watajenga tabia ya kujiamini na kuzifikia ndoto zao.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi Neema Msitha ameitaka jamii kuwapa nafasi wasichana kushiriki katika michezo jambo ambalo litawasaidia kuwaondolewa vishawishi na kunyanyua ushiriki wao katika michezo.
Naye balozi wa Japan nchini Tanzania, Yasushi Misawa amesema mashindano ya Ladies First awamu ya sita iwe sehemu ya jukumu jamii kupigania haki za wasichana katika michezo.
Amesema hawatakuwa tayari kurudia makosa ya zamani kwa kutowapa nafasi wasichana katika sekta ya michezo ambayo kwa sasa inaongoza kufanya vizuri wa wanawake.
“Tupo katika jamii inayobadilika haraka na wanawake wanachangia kufanya mabadiliko hayo, kuwapa elimu na michezo inachangia katika jamii.
Kuna mipango mingi ya kusaidia wanawake katika ndoto zao na wanaume wanaweza kukuza na kuchangia maarifa yao,” amesema.
Baadhi ya mikoa ambayo itashiriki katika mashindano ya Ladies First ni Dar es Salaaam, Ruvuma, Kilimanjaro, Tanga, Dodoma, Mara, Singida Lindi, Mtwara, Simiyu, Ruvuma, Iringa, Unguja Magharibi na Pemba