Michezo MingineRiadha

Majaliwa ahamasisha wananchi kushiriki michezo

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewahamasisha wananchi kwenye maeneo mbalimbali nchini kushiriki katika michezo kwa kuwa ni ajira, uchumi na huimarisha afya.

Majaliwa amesema leo baada ya kuzindua mbio za hisani, Ruangwa Marathon katika kiwanja cha Kilimahewa kilichopo wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi.

“Tunapa faida nyingi kwa kufanya michezo, tushiriki katika michezo pamoja na kukimbia riadha kwa kuongeza vipaji tulivyonavyo kwani tukishindana tunapata na zawadi. Michezo ni uchumi,” amesema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Molel amesema mazoezi yanasaidia katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Dkt. Molel amemshukuru Waziri Mkuu kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika mbio hizo za hisani zilizokuwa na lengo la kukusanya fedha kwa ajili ya kununulia vifaa tiba wilayani Ruangwa.

Related Articles

Back to top button