Kwingineko
Ole Solskjaer ateuliwa kuifundisha Besiktas

ISTANBUL:MKURUGENZI wa Ufundi kutoka Norway Ole Gunnar Solskjaer, sasa ni kocha mpya wa Besiktas baada ya kufikia makubaliano ya kuongoza timu hiyo hadi mwaka 2026.
Solskjaer aliwasili jijini Istanbul ambapo alipokelewa na Makamu wa Rais wa Besiktas, Hakan Daltaban, pamoja na viongozi wengine wa klabu katika Uwanja wa Ndege wa Atatürk.
Akizungumza na wanahabari mara baada ya kuwasili, Solskjaer alisema:
“Nimefurahi sana kuwa hapa. Ni jambo la kipekee kuona watu wengi wamejitokeza kwa ajili ya klabu hii kubwa. Tayari tumefanya mikutano ya awali, na natarajia kwa hamu kuanza kazi yangu. Ni heshima kubwa kuwa katika jiji hili maridadi.”
Solskjaer aliwahi kuzifundisha klabu kadhaa zikiwemo Molde (2015-2018) na Manchester United (2018-2021).