Huyu baba ana balaa huyo!

LONDON, ENGLAND: WINGA wa Arsenal,Raheem Sterling ameweka rekodi ya kuwa Mwingereza wa kwanza kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na timu nne tofauti za England yaani Arsenal, Manchester City, Liverpool na Chelsea.
Sterling mwenye miaka 29 aliyejiunga Arsenal akitokea Chelsea mwanzoni mwa msimu huu aliweka rekodi hiyo katika mchezo wa klabu yake hiyo mpya dhidi ya Atalanta alipochukua nafasi ya Bukayo Saka dakika ya 73.
Winga huyo alicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya September 17, 2014 akiwa Anfield Liverpool ikiichapa Ludogorets Razgrad mabao 2-1. Kisha kucheza tena akiwa kikosi cha Manchester City Septemba 15, 2015 ambapo Manchester city walipoteza 2-1 mbele ya Juventus.
Akiwa Chelsea Sterling alicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya September 6, 2022 dhidi ya Dinamo Zagreb, Chelsea ikichapwa 1-0 ugenini
Hata hivyo hakuna timu kati ya hizo zilizotwaa ubingwa wa Ligi hiyo Sterling akiwa sehemu ya kikosi katika msimu wake wa kwanza.
Akiwa Liverpool msimu wa 2014-2015 Liverpool waliondolewa katika hatua ya makundi. Msimu uliofuata (2015-2016) akiwa Manchester City klabu hiyo iliondoshwa na Real Madrid kwenye nusu fainali
Baada ya kuhamia London msimu jana akiwa na Chelsea, klabu hiyo iliishia hatua ya robo fainali kwa kufurushwa na Real Madrid. Msimu huu yupo Arsenal na tayari amecheza mchezo wake wa kwanza na Arsenal wamepata suluhu dhidi ya Atalanta.