Bayindir nyanda mpya Man Utd

KLABU ya Manchester United imemsajili golikipa wa Uturuki, Altay Bayindir kutoka timu Fenerbahce kwa ada ya pauni milioni 4.3 sawa na shilingi 13.3.
Bayindir mwenye umri wa miaka 25 ambaye amecheza mechi tano timu ya taifa ya Uturuki amejiunga na United kwa mkataba wa miaka minne.
“Ni heshima kubwa kujiunga na Manchester United na kuwa mchezaji wa kwanza wa Uturuki kucheza klabu hii yenye maajabu,”Bayindir.
Usajili wa Bayindir unafuatia kuondoka kwa golikipa Dean Henderson, ambaye amejiunga na Crystal Palace kwa ada ya pauni milioni 20.
Bayindir anakuwa golikipa wa pili kujiunga na United majara haya ya kiangazi baada ya usajili mcameroon Andre Onana kutoka Inter Milan kwa pauni milioni 47.2
Aidha Bayindir anakuwa mchezaji wa nne kusajiliwa Old Trafford majira haya ya kiangazi baada ya kiungo Mason Mount akitokea Chelsea, mshambuliaji Rasmus Hojlund kutoka Atalanta na Onana.