Ligi Kuu
Mwalimu anatakiwa nyumbani
DAR ES SALAAM: UONGOZI wa timu ya Singida Black Stars umeanza kumtolea macho mshambuliaji wao Suleman Mwalimu naekipiga kwa mkopo Fountain Gate FC.
Mwalimu ameonesha kiwango kizuri cha kutikisa nyavu ndani ya michezo mitatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Singida Black Stars, Hussein Massanza ni kuwa Black Stars wamefurahishwa na kiwango kinachooneshwa huyo.
“Tunamfatilia kwa ukaribu mchezaji wetu huyo, hii ni mara ya kwanza anacheza Ligi Kuu Bara, lakini ameanza kuonesha makali yake mapema,” amesema Massanza.
Ameongeza kuwa kulingana na kiwango alichokionesha akiwa visiwani Zanzibar walishawishika kumsajili na kisha kumpeleka kwa mkopo Fountain Gate FC ambapo amekuwa msaada ndani ya timu hiyo.