Ligi Kuu

Instagram yamponza Ali Kamwe

DAR ES SALAAM: Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya bodi ya ligi kuu (TPLB) imempeleka kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Ofisa Habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe sambamba na Ofisa Habari wa klabu ya Kagera Sugar, Hamis Mazanzala kwa tuhuma za kutenda makosa ya kimaadili kupitia machapisho yao kwenye kurasa za mtandao wa kijamii wa Instagram.

Inadaiwa kuwa Ali Kamwe kupitia mitandao yake ya Kijamii alichapisha maandiko kinyume na Maadili ya Viongozi na Maofisa wa Klabu ambayo yanadaiwa kuleta uchonganishi na kuchafua taswira ya mpira wa Tanzania.

Taarifa iliyotolewa na bodi ya ligi imewakumbusha pia Maofisa Habari au Wasemaji wa klabu zote kuzingatia kanuni za Ligi na za maadili wakati wote wanapotekeleza majukumu yao ili kuepuka kutoa kauli ambazo zinaweza kuzua chuki, taharuki au kuchochoea vurugu viwanjani.

Related Articles

Back to top button