Ligi Kuu
Maji yameanza kujitenga na mafuta?

BABATI: KLABU ya Simba imeshindwa kufurukuta katika dimba la Tanzanite Kwara, kwa kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Fountain Gate FC , mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Bao la limefungwa na Leonel Ateba dakika ya 57 kazi nzuri iliyofanywa na Ladaki Chasambi dakika 75 nyota huyo amejifunga akirudish mpira wa kipa wake, Moussa Camara amemshinda kuingia nyavu.
Kwa matokeo hayo Simba inakuwa na alama 44 na kushindwa kurejea kilele na kumuacha Yanga akiendelea kusalia kuongoza msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 45.
Mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkubwa ndani ya dakika 45 ya kipindi cha kwanza timu hizo zlimeenda mapumziko ikiwa 0-0.