Ligi Kuu

Ahmed: Tabora UTD watatutambua!

DAR ES SALAAM: MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema wataionesha Tabora sababu ya kubaki katika michuano ya kimataifa.

Ahmed amesema kikosi chao kinaendelea na mazoezi kujiandaa na duru ya pili na wanahitaji kuendeleza walipoishia kwa kutafuta alama tatu muhimu katika michezo iliyopo mbele yao ikiwemo mechi yao dhidi ya Tabora United.

Amesema wanatambua hautakuwa mchezo rahisi lakini wamejipanga kuhakikisha wanaendelea kupata matokeo kwa ajili ya kufikia malengo yao ya msimu huu wa kuwapa furaha mashabiki wao.

“Nilikuwa najiuliza Tabora United wamepata wapi usajili wa kututambia, kumbe utamu waliopata kutoka kwa nyuma mwiko na kijana wa mbande ndio unampa jeuri akidhani kila mtu ana mmudu???tutawaonyesha kwanini Simba pekee yetu tupo robo fainali,” amesema

Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi ya mchezo huo wa kiporo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United Jumapili, Februari 2, Uwanja wa Al Hassan Mwinyi, mjini Tabora.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button