Moto waahirisha tangazo la albamu ya Beyonce

LOS ANGELES: MWANAMUZIKI anayetamba na wimbo wa ‘Texas Hold ‘Em’ Beyonce Knowles ameahirisha tangazo lake la ujio wa albamu yake mpya ya ‘Cowboy Carter’, kutokana na uharibifu uliosababishwa na moto wa California, hivyo atatoa tangazo hilo siku nyingine.
Katika taarifa yake kwenye ukurasa wake rasmi wa Instagram, Beyonce alisema: “Tangazo la Januari 14 litaahirishwa hadi tarehe nyingine kutokana na uharibifu uliosababishwa na moto wa nyika unaoendelea kuzunguka maeneo ya Los Angeles.
Ninaendelea kuomba kwa ajili ya uponyaji na kujenga upya familia zinazoteseka kutokana na kiwewe na hasara. Tumebarikiwa sana kuwa na wajibu wa kwanza jasiri ambao wanaendelea kufanya kazi bila kuchoka kulinda jamii ya Los Angeles.
Beyonce mwenye miaka 43, alifichua kwamba alikuwa ametoa dola milioni 2.5 kusaidia juhudi za misaada huko Los Angeles.
Aliongeza: “Hazina ya Usaidizi wa Moto ya taasisi yake ya ‘BeyGOOD’ imetoa dola milioni 2.5 kusaidia moja kwa moja familia zilizopoteza nyumba zao na mashirika ya kijamii yliyo mstari wa mbele kwa kutoa misaada. Tafadhali ungana nasi katika kuunga mkono kwa chochote unachoweza.
Mshindi huyo wa Grammy alitangaza pesa hizo zitatolewa kwa Mfuko wa Msaada wa Moto kupitia Taasisi yake ya BeyGOOD.
Ujumbe uliotumwa kwenye ukurasa wa Instagram wa hisani ulisema: “Los Angeles tunasimama nawe. BeyGOOD inachukua hatua kwa kutangaza msaada wa Moto kwa mchango wa dola milioni 2.5.
Beyonce pia wiki iliyopita alihairisha tamasha lake katika ukumbi wa Rose Bowl huko Pasadena, California, na kuchelewesha albamu yake mpya ya ‘Hurry Up Tomorrow’ kwa heshima kwa wale walioathiriwa na moto.
Moto wa nyika wa California umeua watu 24, kuharibu jamii kadhaa na zaidi ya miundombinu 12,300 ndani ya ekari 40,000 za eneo la Greater Los Angeles huku kukiwa na taarifa za kuwahamisha wakazi 92,000.