KwinginekoSerie A
Mitanange Ligi Kuu Italia, FA England
MECHI za Ligi Kuu Italia na Kombe la FA England zinaendelea leo kwa michezo kadhaa.
Katika Ligi Kuu Italia Inter itakuwa nyumbani kuikaribisha Atalanta wakati Napoli itakuwa ugenini dhidi ya Sassuolo.
Huko England, patashika ya Kombe la FA raundi ya 5 Chelsea itakuwa mwenyeji wa Leeds United wakati Manchested United itakuwa mgeni wa Nottigham Forest.
Wolves na Brighton zitaonesha kazi Wolves ikiwa mwenyeji wakati Southampton ni mgeni wa Liverpool.