EPL
Liverpool yahamia kwa Zubimendi
LIVERPOOL wanahaha kumnunua kiungo wa kati wa Real Sociedad, Martin Zubimendi huku wakipania kufanya usajili wao wa kwanza chini ya meneja mpya Arne Slot.
Zubimendi alikuwa sehemu ya kikosi cha Hispania kilichoshinda Euro 2024 na aliingia kipindi cha pili kama mbadala wa Rodri England ikifungwa 2-1 katika mchezo wa fainali.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekuwa Sociedad tangu 2011 na ana kifungu cha kutolewa chenye thamani ya euro 60m (£51.5m).
Zubimendi aliisaidia Sociedad kumaliza nafasi ya sita msimu uliopita, akifunga mara nne katika mechi 31 za ligi.
Kama Liverpool itamnasa Zubmendi,atakuwa ni mchezaji wa kwanza kuwasili chini ya Slot, ambaye alichukua mikoba ya Jurgen Klopp.