EPLKwingineko

777 Partners kuinunua Everton

KLABU ya Everton ‘The Toffees’ ya Ligi Kuu England(EPL) inayosuasua inakaribia kuuzwa kwa kampuni ya uwezekani ya Miami, Marekani, 777 Partners.

The Toffees iliyokumbwa na matatizo ya kifedha ilirejea kwenye mazungumzo na kampuni ya uwekezaji yenye makao yake makuu Miami, Marekani baada ya mazungumzo na MSP Sports Capital kuvunjika mwezi Agosti.

Kwa mujibu wa tovuti ya BBC ununuzi huo utamaliza umiliki wenye msukosuko wa mmiliki klabu hiyo, Farhad Moshiri, ambaye aliwekeza kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016.

Chanzo cha habari cha karibu na Moshiri kimesema Everton imetafuta uwekezaji kwa muda, lakini mpango huo bado haujakamilika.

Everton inayonolewa na kocha Sean Dyche ipo nafasi ya 18 katika msimamo wa EPL baada ya kujikusanyia pointi moja hadi sasa baada ya michezo mitatu ya msimu huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button