BundesligaEPLKwingineko

Rasmi Kane ni mwanabavaria

NAHODHA wa England, Harry Kane, amejiunga na mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich kwa mkataba wa miaka minne akimaliza rekodi yake kucheza Tottenham.

Mshambuliaji huyo amesaini dili lenye thamani ya zaidi ya Euro milioni 110 sawa na shilingi bilioni 295 na anaweza kucheza katika mechi ya Super Cup Ujerumani dhidi ya RB Leipzig leo.

Kane mwenye umri wa miaka 30 anaondoka Spurs inayoshiriki Ligi Kuu England(EPL) kama mfungaji wao bora akiwa na magoli 280 katika michezo 435.

Katika mitandao ya kijamii ameandika “anahisi huu ni wakati wa kuondoka” Spurs.

Hatma ya Kane imekuwa katika utata msimu wote kwa sababu alikuwa amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake Spurs.

“Nina furaha sana kuwa sehemu ya FC Bayern sasa,” amesema Kane ambaye atavaa jezi namba 9 Bayern na amesaini hadi 2027.

Ameshinda kiatu cha dhahabu EPL 2015-16, 2016-17 na 2020-21 akifunga mabao 213 katika michezo 320 ya ligi hiyo.

Related Articles

Back to top button