EPL

Man United, kama msimu uliopita tu

Huenda klabu ya Manchester United ikakumbwa na pigo jingine la majeruhi katika michezo ya kirafiki inayowaandaa na msimu mpya baada ya Marcus Rashford kuumia na kutoka nje katika ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Real Betis, huko San Diego, California.

Mshambuliaji huyo alionekana kuumia kifundo cha mguu baada ya kuchezewa rafu na Sergi Altimera na baada ya hapo akaelekea moja kwa moja katika vyumba vya kubadilishia nguo.

Naye Winga wa klabu hiyo, Antony alionekana kupata jeraha licha ya kuingia dakika ya 62 lakini akaishia kutolewa dakika ya 86 baada ya kushindwa kuendelea na mchezo.

Baada ya mchezo huo, Rashford alionekana akiwa na mashabiki akisaini jezi zao na vitabu lakini Manchester United wanasubiri kuona kama ataungana na Rasmus Hojlund pamoja na Leny Yoro katika orodha ya majeruhi.

Hojlund atakuwa nje ya dimba kwa muda wa wiki 6 na hivyo kukosa michezo minne ya mwanzo wa msimu mpya huku Yoro akiripotiwa kukosa michezo 9.

Hili ni pigo kwa kLabu hiyo kwani msimu uliopita United walikuwa na kesi za majeruhi pamoja na ugonjwa zipatazo 66, kitu kilichoathiri msimu wao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button