Tottenham vs Liverpool hakuna TAA

BOSI wa Liverpool Arne Slot amesema beki wake wa kulia Trent Alexander-Arnold ataukosa mchezo wa marudiano wa nusu fainali ya Carabao Cup dhidi ya Tottenham Hotspur kesho Alhamisi dimbani Anfield
Trent-Alexander Arnold alifanyiwa mabadiliko ya lazima mnamo dakika ya 70 ya mchezo wa ligi kuu waliopata ushindi wa 2-0 mbele Bournemouth Jumamosi kwa kile kinachodhaniwa kuwa ameumia nyama za paja
“Ataukosa mchezo huu. Tutaona kama atacheza Jumapili lakini uhakika ni kwamba hatakuwepo kesho. Aliondoka uwanjani na maumivu lakini tayari amerudi kwenye uwanja wa mazoezi si na wachezaji bali kocha wa viungo hivyo tuwe na subira tuone ni mda gani atachukua” – Amesema Slot
Liverpool ambao wanatetea ubingwa wa kombe hilo walilotwaa na Jurgen Klop msimu uliopita watakuwa nyumbani kusaka nafasi ya fainali huku wakiwa na kazi nyepesi ya kupindua ushindi wa 1-0 wa Tottenham katika mzunguko wa kwanza. Mchezo huo kama ule wa leo wa Arsenal na Newcastle utapigwa majira ya saa 5 usiku saa za Afrika Mashariki.