Gamondi aitega Simba

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi amesema licha ya kuwepo kwa mapumziko ya wiki mbili kupisha michezo ya timu za Taifa kambini kwake hakuna mapumziko bali anatumia muda huo kutengeneza mitego kuelekea mchezo wa dabi dhidi ya Simba, Oktoba 19.
Amesema amekuwa akizifatilia kila mechi za wapinzania wao, ikiwemo Simba wanaokutana katika mchezo unaofuatia wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
“Hiki ni kipindi cha mapumziko ya wiki mbili ambazo natumia kwa ajili ya kuwasoma wapinzani wetu tunatarajia kukutana nao Oktoba 19, malengo yetu ni kushinda. Tunafahamu wapinzani wetu wako vizuri pamoja na benchi la ufundi.
Haitakuwa mechi rahisi kwa kuwa mechi iliyopita walipoteza, hawatakuja kama ilivyokuwa mara ya kwanza nimezungumza na wachezaji wangu kujiandaa kwa ajili ya mchezo ujao,” amesema Gamondi.
Ameongeza kuwa wanatambua muda sio rafiki kwa sababu wachezaji wake wengi wapo kwenye majukumu ya timu za Taifa na wakirudi watakuwa na muda mfupi wa kujiandaa na mchezo huo lakini ataendelea kusuka mipango yake kwa kutumi