Ligi Kuu

Pacome Zouzoua: Ushindi dhidi ya Tabora United watupa hamasa mpya

DAR ES SALAAM: KIUNGO wa Yanga, Pacome Zouzoua, amesema ushindi wao dhidi ya Tabora United ni hatua muhimu inayowapa motisha kwa michezo ijayo, ikiwemo dhidi ya Coastal Union na Azam FC.

Pacome ameeleza kuwa kila mchezo ni mgumu, lakini wao kama wachezaji wanajitahidi kupambana uwanjani ili kupata matokeo mazuri na kufanikisha malengo yao msimu huu.

Nyota huyo amefikisha jumla ya pasi nane za mabao katika ligi, akishikilia nafasi ya pili kwenye orodha ya wachezaji wenye pasi nyingi za mabao, huku kinara akiwa ni Feisal Salum wa Azam FC mwenye pasi 12.

“Kazi bado inaendelea, na furaha yetu ni kuona tunapata ushindi. Mchezo wetu dhidi ya Tabora United haukuwa rahisi, tulikutana na timu yenye wachezaji wazuri na tulilazimika kupambana sana,” amesema Pacome.

Ameongeza kuwa ushindi huo unawapa motisha zaidi kwa ajili ya michezo miwili ijayo, ambayo inatarajiwa kuwa migumu dhidi ya Coastal Union na Azam FC.

“Tunahitaji kujituma zaidi na kujiandaa kwa michezo hiyo, kwani tunajua haitakuwa rahisi,” amesema kiungo huyo.

Related Articles

Back to top button