Ligi Kuu

Ishu ya Mzize ndio kwanza imeanza!

DAR ES SALAAM: UONGOZI wa Yanga umesema hautamuuza Mshambuliaji Clement Mzize bali ataendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kwa misimu mingine.

Ofisa habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema hakuna klabu au timu inayoweza kumnunua Mzize kwa sababu bado yupo kwenye mipango ya klabu hiyo.

Amesema mshambuliaji huyo mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu na wako kwenye mipango ya kumuongeza kwa sababu ni tegemeo kwa nyota wazawa.

Amesisitiza kuwa hawana mpango wa kuachana na wachezaji wao muhimu hali iliyosababisha kutoa kiasi kikubwa cha fedha kumbakiza kiungo wao Stephane Aziz Ki.

 

Related Articles

Back to top button