Ligi Kuu

Kocha Fadlu hapoi, kazi kazi

DAR ES SALAAM: KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids hataki masihara hata kidogo kwani ameamua kukatiza mapumziko kwa wachezaji wake baada ya kufanikiwa kutafuta mechi ya kirafiki ya Kimataifa wanayotarajia kucheza dhidi ya Al Hilal ya Sudan Agosti 31, Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.

Baada ya mchezo dhidi ya Fountain Gate FC, Jumapili, Agosti 25, wachezaji walipewa mapumziko ya siku mbili na leo wanaingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Al Hilal, Ligi inasimama kupisha timu za Taifa kucheza michezo ya kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika ( AFCON).

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally, amesema kikosi kinaingia kambini leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal.

Amesema asilimia kubwa ya mchezo umekamilika kilichopo kwa sasa ni maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa mashabiki wao.

“Wachezaji wamepewa mapumziko baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Fountain Gate wanarejea kambini kuanza maandalizi ya mchezo huo rasmi, dhidi ya Al Hilal ya Sudan kila mmoja anafahamu umaarufu wao, mchezo utachezwa saa 10: 00 jioni huu ni uwanja wetu wa nyumbani,” amesema Ahmed.

Ametangaza viingilo kwenye mchezo huo wa kimataifa  Sh 10,000 kwa mzunguko na 20,000 VIP, amesema viingilio hivyo ni kutokana na hadhi ya mchezo huo na hadhi ya mpinzani wao.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button