Dogo Rema aomba sapoti ya mashabiki

DAR ES SALAAM: MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Dogo Rema, amewaomba mashabiki wake kuendelea kumsapoti katika kazi zake za muziki pamoja na kumpatia fursa za kushiriki katika maonesho mbalimbali.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, msanii huyo ameeleza kuwa mafanikio aliyoyapata yametokana na mchango mkubwa wa mashabiki wake waliomuinua kutoka maisha ya kawaida hadi kufikia hatua ya kuwa mwakilishi wa vijana wengi wanaotoka katika mazingira magumu.
“Ndugu zangu, nyie ndio mmenitoa mtaani na mkaamua niwe mwakilishi wa vijana wote wanaotokea katika maisha magumu.
Pia mkanijengea imani ya kwamba naweza kufikia ndoto zangu licha ya changamoto tulizopitia,” ameandika Dogo Rema.
Aidha, ameongeza kuwa kwa imani na upendo huo, anaomba kuendelea kupewa sapoti kupitia show na mialiko mbalimbali ili aweze kujikimu kimaisha na pia kusaidia vijana wengine wanaotegemea mafanikio kupitia yeye.




