Ed Sheeran atoka na ‘mpenzi wangu’

NEW YORK: MWANAMUZIKI Ed Sheeran mwenye miaka 34 ametoa wimbo utakaokuwa katika albamu yake ya nane ijayo ya ‘Play’.
Wimbo huo utaachiwa leo jioni ya April 4, sambamba na video ya muziki wa dansi iliyoambatana nayo inayoitwa ‘Pink Heart’.
Akiandika kwenye Instagram yake amesema ‘Azizam’ imetoka sasa, “Nimefurahishwa sana na maoni chanya kwa wimbo huu, na nimefurahishwa sana na mambo mengine ya kustaajabisha niliyofanyiwa.
Mkali huyo wa wimbo wa ‘Shape of You’ hivi majuzi alitania kuwa amefanya video ya wimbo huo nchini Marekani.
‘Azizam’ video ya ‘Pink Heart’ tutaitoa kesho (leo), tulirekodi hii kote Marekani na kidogo katika wimbo wa Ipswich. Ilikuwa hali ya kushangaza popote tulipoenda, nilitaka kutafakari hilo na video pia.
Ed amefanyakazi na mtayarishaji Ilya Salmanzadeh kwenye ‘Azizam’ wimbo unaomaanisha “mpenzi wangu” kwa Kiajemi.
“Niliandika ‘Azizam’ baada ya Ilya kupendekeza muziki wa kuchochewa na urithi na utamaduni wa Kiajemi. Ninapenda kujifunza kuhusu muziki na tamaduni mbalimbali kadiri ninavyosafiri na kuungana na watu.
Albamu hii yote inahusu kucheza, kuchunguza, na kusherehekea. “Wimbo utatoka Aprili 4, na ni mzuri sana. Natumai kila mtu ataupenda pia. Na asante kwa Ilya kwa kunitambulisha kwa ulimwengu na tamaduni nzuri kama hii” amemaliza.