Muziki

Watatu washitakiwa kifo cha Liam Payne

ARGENTINA: UCHUNGUZI wa kifo cha Liam Payne umesababisha watu watatu kushitakiwa kwa kuanguka kwake Oktoba16 kutoka chumba chake cha ghorofa ya tatu katika Hoteli ya CasaSur Palermo huko Buenos Aires nchini Argentina.

Nyota huyo wa zamani wa One Direction mwenye miaka 31 alielezwa kuporomoka kutoka futi 45 hadi kifo chake katika hoteli hiyo.

Mwendesha mashitaka wa umma wa Argentina ametangaza katika taarifa jana Alhamisi Novemba 07, 2024 kwamba watu watatu wamefunguliwa mashtaka kuhusiana na kifo hicho.

Watu hao wanadaiwa kushitakiwa kwa kumtelekeza mwanamuziki huyo hadi kifo chake, taarifa kutoka ofisi ya mwendesha mashitaka Andres Esteban Madrea imethibitisha.

Mtuhumiwa wa kwanza anayeshikiliwa na polisi ni rafiki wa msanii huyo aliyekuwa akiambatana na mwanamuziki huyo kila siku wakati alipokuwa akiishi nchini Argentina.

Mfanyakazi wa hoteli hiyo pia anashutumiwa kwa kumpa Payne kokeini mara mbili alipokuwa akikaa hotelini hapo, taarifa hiyo imesema.

Na mtu wa tatu aanayeshikiliwa ni msambazaji wa dawa za kulevya zilizokutwa chumba alichokuwa mwimbaji huyo aliyekuwa katika chumba hicho tangu Oktoba 14.

Madrea amethibitisha kwamba watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa vitendo viwili; kila mmoja vya kusambaza dawa za kulevya.

Ofisi ya mwendesha mashitaka imeongeza kwamba ilisikiliza ushuhuda mwingi na wamechambua muda wa video za CCTV pamoja na simu ya Liam, ambayo ilihusisha ujumbe na akaunti za mitandao ya kijamii.

Habari za mashitaka ziliibuka baada ya kubainika kuwa mwili wa Liam umesafirishwa hadi nyumbani kwao nchini Uingereza kabla ya mazishi yake, ambayo inaelezwa yatafanyiwa maombi katika kanisa kuu nchini humo.

Gazeti la The Sun liliripoti kuwa baba yake Liam, Geoff Payne,66, alikuwa kwenye ndege kuelekea Heathrow akiwa amebeba mabaki ya mwanawe, na liliripoti kuwa mwili huo umehamishiwa katika mji wa nyumbani wa Liam wa Wolverhampton.

Related Articles

Back to top button