MSANII Tessy Chocolate ambaye ni mzazi mwenzake msanii wa Bongo fleva Aslay Isiaka amesema familia ni bora kuliko umaarufu.
–
Tessy amesema umaarufu sio bora kuliko familia, hivyo yeye anachojali zaidi ni kuhusu familia ndio maana anampa ushirikiano Aslay katika shughuli zake za Muziki.
–
“Lazima nimpe ushirikiano baba mtoto wangu katika kuelekea miaka kumi ya Aslay tulikuwa pamoja nyimbo 100 pale Where House Masaki September 30 familia ni bora kuliko umaarufu.” amesema Tessy.
–