Baada ya kununua gari ‘Dem wa Facebook’ akana kupata ajali
NAIROBI: MCHEKESHAJI Kotoka Kenya Marufu Kwa Jina la ‘Dem wa Facebook’ amekanusha tuhuma za kwamba amepata ajali na hali yake ni mbaya baada ya kukimbizwa hospitalini.
Katika chapisho lake kwenye mtandao wa Instagram amewahakikishia mashabiki wake kwamba taarifa hizo ni za uongo, yeye yupo salama na hajapata ajali yoyote.
“Habari zenu,” alianza katika ukurasa wake wa Instagram akijirekodi video akiwa ghorofani huku akionesha picha ya gari jekundu.
“Nina furaha kila wakati, lakini leo nimekatishwa tamaa sana. Watu wangu, kwa huruma, sijapata ajali. Sijawahi kupata ajali yoyote. Watu wananipigia simu, wakiniuliza niko hospitali gani? au nina majeraha gani?”
Uvumi huo wa uwongo ulisambaa baada ya mchekeshaji huyo kuonesha gari lake jipya alilonunua ikiwa ni sehemu ya mafanikio yake lakini gari hilo lilionekana kubondeka sehemu moja ndipo watu wakatoka na taarifa kwamba amepata ajali bila kujua lilikuwa gari lake alilonunua.
Dem wa Facebook amesema uvumi huo pia ulikuwa umesababisha wasiwasi miongoni mwa wanafamilia yake, huku mama yake akiingiwa na huzuni mkubwa. “Mama yangu akiwa na huzuni mkubwa alipiga simu yangu kuhakikisha kama nimepata ajali baada ya kuzimia alipopata taarifa hizo,” ameeleza Dem wa Facebook.
Mchekeshaji huyo ameshauri watoa taarifa wawe wanathibitisha kwanza habari kabla ya kuitangaza mitandaoni.
Taarifa hizo zilizagaa mitandaoni wakati Dem waa Facebook akiwa anasherehekea kupata gari lake la kwanza lenye rangi nyekundu. Amesherehekea gari hilo akiwa na marafiki zake wa karibu huku wimbo wa msanii mwenzake wa Kenya Otile Brown ‘Ni Wote’ ukiwaburudisha Pamoja na kupokea pongezi kutoka kwa wadau wa sanaa nchini humo.