Mastaa

Victor Osimhen alalamikiwa ‘kumblock’ promota

LAGOS: MCHEKESHAJI na promota wa filamu nchini Nigeria, Jollof, amemlalamikia mshambuliaji wa Super Eagles, Victor Osimhen kwa madai kwamba amemblock katika mtandao wa Instagram kutokana na ugonvi wa mchezaji huyo na kocha Finidi George.

Mchekeshaji huyo alidai kuwa Osimhen alimblock baada ya kumkosoa kutokana na ugomvi wa hadharani uliotokea hivi karibuni kati ya mchezaji huyo na kocha wa Super Eagles, Finidi George.

Mchekeshaji huyo alibainisha kwamba hajawahi kumuomba chochote wala kumfanyia ubaya wowote kiasi cha kuchukua jukumu la kumblock kwenye mitandano yake ya kijamii ikiwemo Instagram.
Akinukuu video hiyo, aliandika, “Mchezaji wa msimu mmoja wa maajabu Victor Osimhen ameniblock kwenye Instagram! Naam, sihitaji aende popote maishani kwake.

“Kwa hivyo ikiwa haukupenda jinsi nilivyokusahihisha. Nimekua na umri wa miaka 12. Unahisi ukinizuia nitakufa? Je, nimefaidika chochote kutoka kwako? Sijawahi kukuuliza chochote wala, sihitaji chochote kutoka kwako.” Alimaliza mchekeshaji huyo.

Katika video iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Jollof alimkumbusha Osimhen kuhusu tofauti ya umri kati yao.

Hata hivyo mchezaji Osiemen hajaandika chcochote kuhusu tuhuma za mchekeshaji huyo wala kocha wake wat imu ya taifa Finid George.

Related Articles

Back to top button