Mastaa

Usher afuta maonyesho yake ya Florida kutokana na Kimbunga Milton

FLORIDA: MWANAMUZIKI Usher amesitisha matamasha yake yajayo huko Miami baada ya maafisa huko Florida kutangaza hali ya hatari kutokana na kimbunga Milton.

Ushera ameeleza kwamba ameamua kufutilia mbali maonyesho yake katika Kituo cha Kaseya cha Miami kwa sababu za usalama.
Dhoruba ya kitropiki imepandishwa hadhi na kuwa ya aina tano ya vimbunga vyenye nguvu zaidi na inatabiriwa kupiga pwani ya kusini magharibi ya jimbo hilo huku zaidi ya wakazi milioni moja wakitakiwa kuhama.

Katika chapisho kwenye ukura wake wa Instagram, mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 45 aliandika: “Maonyesho yangu yajayo huko Miami katika Kituo cha Kaseya yamepangwa tena Desemba kwa sababu ya hali ya hatari huko Florida.

“Usalama na ustawi wa kila mtu vinasalia kuwa kipaumbele changu kikuu na ningependelea kusherehekea nanyi nyote mkifika na kutoka salama katika onyesho langu. Tunawaombea wote walioathiriwa na janga hili la asili.”

Aliongeza kwa maelezo: “Florida, kaa salama. nitakuona hivi karibuni.”
Maonyesho ya Usher yalikuwa yamepangwa kufanyika Oktoba 11, 12 na 14 na sasa yanatarajiwa kufanyika Desemba 16, 18 na 19 katika ukumbi huo huo.

Kimbunga Milton kinakuja wiki chache tu baada ya kimbunga Helene kusababisha uharibifu huko Florida.
Rais wa Marekani Joe Biden ameahirisha safari iliyopangwa kwenda Ujerumani na Angola ili aweze kusimamia maandalizi ya dharura na akawaonya wakaazi katika eneo hilo wahame haraka: “Ni suala la maisha na kifo,

“Hii inaweza kuwa dhoruba mbaya zaidi kupiga Florida katika zaidi ya karne moja na haitakuwa hivyo, lakini inaonekana hivyo hivi sasa.”
Gavana wa Florida Ron DeSantis pia alionya juu ya hatari inayokabili serikali, akisema: “Wacha, lakini lazima tujitayarishe kwa makubwa yanayotokana na athari kwa pwani ya magharibi ya Florida”.

Related Articles

Back to top button