Mastaa

Jung Woo Sung akubali mtoto akataa ndoa na Moon GaBi

KOREA KUSINI:Jung Woo Sung amekiri kuwa yeye ni baba wa mtoto kwa mwanamitindo, Moon Gabi lakini amekataa kumuoa mwanamitindo huyo jambo ambalo limewakera mashabiki wa msanii huyo kiasi kwamba wamemtupia maneno ya kumkashifu nyota huyo wa tamthilia ya K.

Tamthilia ya maisha halisi ya mwigizaji Jung Woo Sung imeibua sintofahamu baada ya taarifa ya vipimo vya daktari kufichua kuwa yeye ndiye baba wa mtoto wa mwanamitindo huyo ingawa hataki kumuoa mama wa mtoto huyo.

Novemba 24, wakala wa Jung Woo Sung’s Artist Company ilithibitisha pia taarifa hizo za ikidai muigizaji wao alikuwa baba wa mtoto wa mwanamitindo huyo mara tu mwanamitindo huyo alipotoa tangazo la kushtukiza kwenye ukurasa wake wa Instagram akifichua kwamba alikuwa mama wa mtoto wa kiume.

Moon Gabi aliandika wakati huo, “Sikuwa tayari hata kidogo kwa habari hii iliyonijia ghafla, hivyo badala ya kujiingiza kikamilifu katika furaha ya ujauzito na pongezi za wengine hadi kuridhika moyoni mwangu, nilitumia muda mwingi wa ujauzito wangu kimya kimya, katikati ya baraka za familia yangu.”

Ameeleza zaidia kwamba: “Nilifanya uamuzi wa kufanya hivyo kwa ajili ya mtoto wangu ambaye bado hajazaliwa. Nilifikiri kwamba ili kulinda kitu chenye thamani ndani ya moyo wangu, nilihitaji kuficha mimba yangu kwa uangalifu mkubwa.

Kampuni ya muigizaji huyo imeendelea kueleza kwamba muigizaji wao Jung Woo Sung ndiye baba mzazi wa mtoto ambaye Moon Gabi amemfichua kwenye mitandao ya kijamii na kwa sasa yuko katika harakati za kujadili njia bora zaidi za malezi ya Watoto huyo na kama baba, atachukua jukumu kamili kwa mtoto wake.

Related Articles

Back to top button