Ligi Daraja La Kwanza

Tamasha la ZIFF 2026 lawaombea nguli wa filamu waliofariki dunia

ZANZIBAR:KABLA ya kuwakaribisha watazamaji kushuhudia filamu ya kufungulia tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar (ZIFF 2026) Juni 24,2026 , Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF, Hatibu Madudu, aliusimamisha ukumbi uliokuwa na zaidi ya watu 300 kwa dakika moja ya ukimya ili kuwakumbuka na kuwaombea wasanii watatu nguli wa tasnia ya filamu Afrika mashariki waliofriki dunia mwaka 2025/26.

Wasanii hao ni Nick Wambugu alikuwa mtayarishaji wa filamu za makala (documentary filmmaker), mpiga picha za video na mwanahabari wa filamu kutoka Kenya, Hashim Kambi, na Mzee Onyango.

Miongoni mwa wadau hao wa filamu walikuwepo viongozi wa kiserikali na wanadiplomasia.

Ukimya huo uliotawala kwa sekunde sitini ulikuwa ni ishara ya heshima ya juu kabisa kwa nguzo hizo tatu za sanaa ambazo zimeacha pengo kubwa lisilozibika katika ulimwengu wa uigizaji na burudani.

Ufunguzi wa msimu wa 29 wa Tamasha uliogubikwa na shamrashamra na mbwembwe za kitamaduni katika Ukumbi wa Wangazija wa Wakfu, ulikumbana na wakati mgumu wa majonzi mazito yaliyobadili sura ya ukumbi huo kuwa ya kipekee na yenye kugusa hisia
Kuguswa kwa tamasha hilo kunatokana na ukweli kwamba wasanii hao hawakuwa wageni wa ZIFF, bali walikuwa na uhusiano wa kina na wa kihistoria na tamasha hili kubwa la sinema barani Afrika.

Mkurugenzi Madudu alikumbusha kwa majonzi kuwa hadi katika msimu uliopita wa tamasha, nguli hawa walikuwa sehemu ya familia ya ZIFF, wakihudhuria, wakichangia mijadala ya kukuza tasnia, na kutembea kwenye jukwaa la tuzo kwa fahari kubwa.
Uwepo wao wa mwisho katika msimu uliopita sasa umebaki kuwa kumbukumbu ya mwisho ya dhahabu, ikidhihirisha namna walivyojitoa maisha yao yote kuhakikisha kuwa filamu za Kitanzania zinapata heshima inayostahili ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Related Articles

Back to top button