Mwigizaji Connie Chiume afariki dunia

CONNIE Chiume, mwigizaji mkongwe raia wa Afrika Kusini ambaye alionekana katika filamu ya Marvel Black Panther, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72, familia yake imetangaza.
Alifariki katika Hospitali ya Johannesburg Jumanne mchana, taarifa fupi ya familia ilisema.
CONNIE Chiume, mwigizaji mkongwe raia wa Afrika Kusini ambaye alionekana katika filamu ya Marvel,Black Panther, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 72, familia yake imetangaza.
“Connie alifariki katika Hospitali ya Johannesburg Jumanne mchana”, taarifa fupi ya familia ilisema.
Chiume aliigiza katika vipindi kadhaa vya televisheni Afrika Kusini vikiwemo Rhythm City, Zone 14 na hivi karibuni katika tamthilia Gomora.
“Familia ya Chiume inasikitika kuwataarifu kuhusu kuondokewa na mwigizaji aliyeshinda tuzo nyingi kimataifa Connie Chiume,” taarifa hiyo ilisema.
Familia imeomba faragha katika kipindi hiki kigumu na ikasema itawasiliana kwa maelezo zaidi baadaye huku mwanae, Nongelo Chiume akimwambia mtangazaji wa TV Newzroom Afrika kwamba alilazwa kwa utaratibu wa matibabu kabla ya kifo chake.
Alipata umaarufu kama mwigizaji mwaka 1989 alipotokea katika kipindi maarufu cha televisheni cha Afrika Kusini ‘Inkom Edla Yodwa’.
Katika filamu ya Black Panther ya 2018, Chiume aliigiza kama Zawavari, mwanachama wa Baraza la Kikabila la Wakanda.