Filamu

Lamata ndoto yangu ilikuwa kuwa askari wa usalama barabarani

DAR ES SALAAM:MWANDISHI na Muandaaji wa Filamu nchini Tanzania, Leah Mwendamseke ‘Lamata’, amefunguka kuhusu ndoto yake ya awali ya kutaka kuwa askari wa usalama barabarani (Traffic Police) kabla ya kujikuta akiingia kwenye tasnia ya filamu.

Akizungumza kuhusu safari yake ya maisha, Lamata alieleza jinsi hali ilivyobadilika na kumlazimu kuchagua mwelekeo tofauti na aliokuwa ameupangilia awali.

“Maisha bwana ni tofauti na unavyotaka. Nilikuwa natamani sana kuwa askari wa usalama barabarani, lakini sasa nimeibukia kuwa mtayarishaji wa filamu hapa Tanzania,” amesema Lamata.

Ameongeza kuwa wakati mwingine mtu anaweza kuwa na ndoto fulani lakini asifanikiwe, hivyo ni muhimu kutafuta njia nyingine ya kufanikisha maisha.

“Unachotamani kuwa usipofanikiwa, angalia njia nyingine, utatoboa kimaisha zaidi kuliko unavyodhania,” amesisitiza Lamata.

Kwa sasa, Lamata anaendelea kufanya vizuri katika sekta ya filamu, ambapo ameandaa na kusimamia miradi mbalimbali yenye mafanikio. Hili ni ushahidi wa jinsi mtu anavyoweza kubadili mwelekeo wa maisha yake na bado kufanikiwa.

Related Articles

Back to top button