Mastaa wa filamu Korea wawavuruga mashabiki
KOREA KUSINI: MWANAMITINDO mashuhuri kutoka Korea Kusini, Jung Ho Yeon na muigizaji nyota katika tamthilia ya ‘K’ na ‘Squid Game’, Lee Dong Hwi wameripotiwa kuachana baada ya kuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa muda wa miaka tisa.
Vyombo vya habari vya Korea Kusini vimeripoti kuhusu kutengana kwa wawili hao huku ikielezwa kuwa, Jung na Lee wameamua kubaki katika hali ya ukarimu kama watu wa ndani ya tasnia, wafanyakazi wenza na marafiki wa muda wote.
Kujibu ripoti hiyo, mashirika ya waigizaji wote wawili yamesema kwamba wawili hao walioachana, wameamua kubaki kama marafiki watakaoshirikiana katika sanaa zao kwa wema na hawakuweka wazi sababu ya kilichosababisha kuachana kwao.
Jung Ho Yeon na Lee Dong Hwi walianza kuchumbiana mnamo 2015 na walitangaza uhusiano wao hadharani mnamo 2016.
Mashabiki wamejitokeza katika kurasa zao wakisikitishwa pamoja na kushangazwa kuachana kwa mastaa hao waliokuwa ndani ya uhusiano kwa miaka tisa.
Jung ameanza masuala ya urembo na mitindo tangu mwaka 2010 ambapo aliingia katika ‘Top Model’ na alipata nafasi ya kutembea katika wiki ya maonesho ya fashioni ya New York mwaka 2016.
Pia amecheza tamthilia ya Netflix iitwayo ‘Squid Game’ iliyotoka mwaka (2021) na ndiyo filamu iliyomtangaza mno katika fani ua uigizaji na kujizolea umaarufu mkubwa ndani ya nje ya Korea Kusini akicheza kwa jina la Kang Sae-byeok.
Mwaka 2013, Lee alikuwa muigizaji bora wa tamthilia za TVN mwaka 2015.