
DAR ES SALAAM: MSANII wa Bongo Fleva na Filamu nchini, Lulu Diva, amemjibu kwa ukali rapa wa Kikosi Kazi, Nikki Mbishi, kufuatia kauli yake kwamba amekuwa akijishikiza kwa msanii D Voice baada ya “kurukaruka” kwa muda mrefu.
Nikki Mbishi alitoa kauli hiyo akizungumzia uhusiano wa Lulu Diva na D Voice, jambo lililomfanya Lulu Diva kutoa majibu makali akimkosoa rapa huyo kwa kuzungumzia maisha yake binafsi.
Kupitia kauli yake, Lulu Diva amesema licha ya Nikki Mbishi kuwa kwenye muziki kwa miaka mingi, bado anatumia muda mwingi kuzungumzia maisha ya watu wengine badala ya kujikita kwenye kazi yake.
“Miaka kibao kwenye game, lakini bado unaishi kwa kuzungumzia maisha ya watu wengine. Wenzako wa kizazi chako wanapanda stage kusherehekea miaka 30 ya kazi, wewe umeshikilia microphone kutengeneza content kuhusu mahusiano yangu.
“Hapo ndipo tofauti ya kuwa legend na kuwa mtu wa zamani inaonekana.”
Lulu Diva pia amegusia suala la umaarufu na mchango wa Nikki Mbishi katika muziki, akisema historia pekee haiwezi kuwa kipimo cha kipaji.
“Na kuhusu game, tusifanye historia kuwa talent. Kuna kizazi kikubwa cha mashabiki wako ambacho ukikiuliza nyimbo zako tatu maarufu, kitatafuta Google kwanza.”
Akimalizia majibu yake, Lulu Diva amemtaka Nikki Mbishi atulie huku akisisitiza kuwa hayuko tayari kuogopeshwa na kauli zake.
“Hebu tulia wewe, Mzeeeee! Cheza unapocheza. Upande huu, mimi sichekeshi. Nakupokea kama ulivyokuja. Huna sharubu yoyote ya kunishtua. Mimi na wewe, ng’ombe!” Lulu Diva




