Ligi Kuu

Yanga wameshatua Kigoma

DAR ES SALAAM:KIKOSI cha Yanga kimewasili mkoani Kigoma leo Juni 11 kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mashujaa utakaochezwa Jumamosi.

Mabingwa hao wa Tanzania Bara walikuwa wakiendelea na maandalizi ya mchezo huo kwa kufanya mazoezi kwenye Uwanja wa KMC kabla ya kuondoka mapema hii leo, wakilenga kujiweka katika hali nzuri ya ushindani kabla ya safari.

Benchi la ufundi la Yanga limeendelea kusimamia programu ya mazoezi inayohusisha kuimarisha utimamu wa mwili, mbinu za mchezo pamoja na marekebisho ya maeneo mbalimbali yaliyoonekana kuhitaji kuboreshwa katika mechi zilizopita.

Mchezo dhidi ya Mashujaa unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku Yanga ikisaka kuendelea kufanya vizuri katika mbio za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu, wakati wenyeji Mashujaa wakitaka kutumia faida ya kucheza nyumbani kupata matokeo mazuri.

Wachezaji wa Yanga wameonesha ari kubwa mazoezini, jambo linaloashiria utayari wa kikosi hicho kuelekea kwenye mchezo huo muhimu wa mwisho wa wiki mjini Kigoma.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button