Ligi Kuu

Fadlu mipango yake raha tupu

DODOMA: KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amesema maandalizi kuelekea mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Dodoma jiji yapo katika hatua nzuri.

Amesema baada ya mchezo uliopita dhidi ya Azam FC, kikosi kilifanya mazoezi ya utimamu wa mwili jana na leo kimesafari tayari kwa mchezo wa kesho.

“Maandalizi yamekamilika na tupo tayari kwa mchezo wa kesho, ratiba ni ngumu lakini tupo na malengo yetu ya ushindi, kikosi kipo kwenye umbo zuri najivunia timu yangu kwa jinsi tunavyocheza,” amesema Fadlu.

Ameeleza kuwa katika mchezo huo atawakosa wachezaji watatu kwa ajili ya majeraha ambao ni Mzamiru Yassin, Yusuph Kagoma na Joshua Mutale kwa mujibu wa daktari hakuumia sana lakini hatuwezi kumtumia kwa sababu ya kuhofia kumuumiza zaidi.

Kwa niaba ya wachezaji, beki wa kulia wa Simba, Kelvin Kijili amesema kwa upande wao wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ingawa amekiri utakuwa mgumu.

“Tupo tayari kwa mchezo wa kesho, tunajua itakuwa mechi ngumu lakini tumejiandaa na lengo ikiwa ni kuchukuwa pointi zote tatu,” amesema Kijili.

Related Articles

Back to top button